Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Ehud Olmert:Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, amesema: "Wazo kwamba mashambulizi ya mapema ya kujikinga yanaweza kuipigisha magoti nchi yenye wakazi milioni 90, na yenye historia ya kale, na ustaarabu wa maelfu ya miaka, ni ishara ya majivuno ya uongo wa wazi na uliombali na ukweli."
"Hata baada ya shambulio la maumivu, lakini bado Iran haitaanguka na bado ina safu ya nguvu kubwa ya makombora."
Amemalizia maoni yake kwa kusema: "Ingawa mashambulizi ya anga ya Marekani kwenye vituo vya nyuklia vya Iran yanaweza kuchelewesha kwa muda mpango wa nyuklia wa nchi hiyo, lakini yatakuwa na matokeo mapana zaidi".
Your Comment